} });
 

 

Aliyekuwa Rais wa Mpito wa Peru, Manuel Merino, ametangaza kujiuzulu wadhifa huo  ikiwa ni siku tano tangu kuchaguliwa baada ya Bunge kumtoa madarakani Rais Martin Vizcarra.

 

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wananchi wa taifa hilo.

 

Merino alitangaza uamuzi huo kwenye televisheni ya taifa na kusema ni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa ambapo tayari mawaziri tisa kati ya 18 wamejiuzulu kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokana na mvutano baina ya polisi na waandamanaji.


Waziri Mkuu wa Peru, Antero Flores-Araoz, amesema Vizcarra ameondolewa kwa mujibu wa sheria, na mtandao wa haki za binadamu umesema watu 112 wameumizwa huku wengine 41 wakiwa hawajulikani walipo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top