} });
 


Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua ilani yake ya uchaguzi ya miaka mitano kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani nchini humo.

Rais Museveni ambaye ni mgombea kutoka chama tawala cha NRM nchini humo, amesema ilani hiyo ya mwaka 2021-2025, inajikita katika vipaumbele vitano ambavyo ni kuongeza ajira, kutoa elimu na huduma za afya, kuhakikisha haki na usawa, ulinzi wa mali na maisha, na kutimiza mwingiliano wa uchumi na siasa.

Rais Museveni amesema, vipaumbele vyake ni ulinzi, upatikanaji wa umeme, ujenzi wa barabara na reli, afya, elimu, na kuwalipa vizuri wanasayansi wa serikali.

Amewataka Waganda wakichague chama cha NRM ili kiendelee kuongoza nchi na kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini Uganda.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top