} });
 

 

Mtanzania aliyehukumiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2015 katika chuo kikuu kimoja nchini Kenya na kusababisha watu 148 kufariki , amejiua mwenyewe akiwa gerezani , vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti.

Washambuliaji wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kenya katika chuo kikuu cha Garissa ,lakini Rashid Charles Mberesero, na wenzake wawili walikamatwa na mwaka jana walihukumiwa kwa kuhusika katika ugaidi.

Hukumu hiyo ilimpa bwana Mberesero kifungo cha maisha gerezani.

Taarifa zinasema alikuwa na matatizo ya akili wakati akiwa gerezani na alikuwa anamuona mtaalamu wa afya akiwa gerezani.

Gazeti la Daily Nation linasema Mberesero alijinyonga mwenyewe aliwa gerezani kwa kutumia blanketi lake.

Shambulio kubwa kutokea mwaka 2015 liliacha simanzi kubwa .

Al-Shabab ilisema imekuwa katika vita na Kenya tangu askari wa Kenya kuingia Somalia mnamo Oktoka 2011.

RASHID CHARLES MBERESERO NI NANI?

Habari kwamba raia mmoja wa Tanzania ni miongoni mwa washukiwa watatu waliopatikana na hatia ya kupanga na kutekeleza shambulio katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya 2015 ziliwaacha wengi na mshangao.

Rashid Charles Mberesero ambaye alikamatwa na watu wengine wanne muda mfupi baada ya mkasa huo wa Garissa uliosababisha vifo vya wanafunzi 148, alipatikana na hatia hiyo wakati mahakama moja nchini Kenya ilipotoa uamuzi wake baada ya takriban miaka minne.

Katika uamuzi huo raia huyo wa Tanzania pamoja na Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa kundi la Al-Shabab.

LAKINI RASHID CHARLES MBERESERO NI NANI HASWA?

Rashid Mberesero, aligundulika katika eneo la tukio akiwa sio mwanafunzi wala mfanyakazi wa chuo hicho.

Kulingana na gazeti la The Citizen toleo la tarehe 10 mwezi Aprili 2016, Rashid aliyesoma shule ya upili ya Bihawana mjini Dodoma alidaiwa kutoroka shule baada ya kukatazwa kuvaa kofia kichwani.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo wakati huo, mwanafunzi huyo alijiunga na shule hiyo mwaka 2015 baada ya kutoka shule ya upili ya Bahi Kagwe.

Chakushangaza ni kwamba licha ya kutoweka katika shule, hakuna aliyefuatilia alikokwenda

Kwa takriban miezi minne wazazi wa kijana huyo walidhani kwamba mtoto wao yupo shule, suala ambalo halikuwa la kweli.

HAIJULIKANI NI NINI HASWA KILIMFANYA KUINGIA KWENYE UGAIDI

Wazazi wa Rashid walishangaa kugundua kwamba kijana wao alikuwa miongoni mwa watu waliopanga na kutekeleza shambulio la Garissa.

Kwa takriban miezi minne wazazi wa kijana huyo walidhani kwamba mtoto wao yupo shule swala ambalo halikuwa la kweli.

Siku za nyuma wakati ambapo kesi ya washukiwa hao ilipokuwa ikiendelea raia huyo alipatikana na ugonjwa wa kiakili akiwa jela.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, Rashid Charles Mberesero aligunduliwa kuwa hawezi kuendelea na kesi baada ya ripoti ya daktari wa maswala ya kiakili kusema kuwa alikuwa akitibiwa tatizo la kuwa na ''mienendo isiyo eleweka'' katika jela ya kamiti.

Kulingana na Daily Nation, upande wa mashtaka ulitaka kupewa muda kujadiliana jinsi ya kuendelea na kesi hiyo dhidi ya wenzake kutoka Kenya.

Alikuwa akikabiliwa na matatizo yasio ya kawaida, ambapo aliamini watu wote karibu naye walikuwa na nia za kishetani'', daktari Mucheru Wang'ombe aliandika katika ripoti yake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top