} });
 


Ni wikiendi ya aina yake kwenye EPL wiki hii. Mzunguko wa 8 utawakutanisha miamba ya soka la Uingereza katika mchezo ambao Manchester City watawakaribisha mabingwa watetezi wa EPL – Liverpool.

 

Mara ya mwisho timu hizi kukutana, “Citizens” waliibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 4-0.

Kwa miaka 5 iliyopita, zimekuwa ni timu zinazofanana kwa idadi ya michezo ya kufungwa na kufunga. Hii inaufanya mchezo wa Manchester City vs Liverpool kuwa mgumu kubashiri.

 

City wapo nafasi ya 10 kwa sasa kwenye msimamo wa EPL wakati Liverpool wanashika nafasi ya 1 wakiwa na pointi 16 baada ya kushinda michezo 5, kutoka sare 1 na kupoteza mchezo 1.

Tukukumbushe kidogo, kwenye mzunguko wa 5, Manchester City waliwafunga Arsenal 1-0. Wakafatia na sare ya 1-1 dhidi ya West Ham na wikiendi iliyopita walishinda 1-0 dhidi ya Sheffield United.

 

Liverpoolwameibuka videdea mara nyingi. Mzunguko wa 6 waliwafunga Sheffield United 2-1 na mchezo wa 7 walishinda 2-1 dhidi ya West Ham.

 

Ila pia tukukumbushe, mzunguko wa 4 ulikuwa wa aibu kwa Liverpool baada ya kufungwa 7-2 na Aston Villa, lilikuwa ni jambo la kushtukiza kwa wapenzi wa soka.

 

Kimsingi, tunapaswa kukumbuka bado ni mwanzoni mwa msimu 2020/21 na Liverpool ni mabingwa watetezi. Mchezo kati ya Manchester City na Liverpool utathibitisha matarajio ya mashabiki wa timu hizi.

 

Pamoja na mchezo huu, kunamichezo mingine kibao inayochezwa kwenye wiki ya 8 kunako Ligi ya Uingereza – EPL, unaweza kujionea odds za michezo hiyo kwa kubofya hapa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top