} });
 


RAIS Mstaafu wa Ghana, Jerry Rawlings (73), amefariki dunia nchini humo kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

 

Jerry Rawlings John AKA J.J. Rawlings ambaye alizaliwa Juni 22, June, 1947 ameaga dunia katika Hospitali ya Korle Bu Teaching, alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Kiongozi huyo aliyetokea jeshini, aliingia katika siasa, na kuwa kiongozi wa Ghana tangu 1981 hadi 2001.  Mwaka 1992 alirejea katika uongozi baada ya mapinduzi ya kijeshi na hivyo kuiongoza Ghana akiwa rais wa kuchaguliwa kidemokrasia mara mbili.

 

Akiwa na cheo cha  ‘flight lieutenant’ katika Jeshi la Anga la Ghana,  alifanya mapinduzi ya kwanza Mei 15, 1979, zikiwa zimebaki wiki tano kabla ya kuirudisha nchi katika utawala wa kiraia.  Mapinduzi hayo yalishindwa na hivyo akahukumia kifo.

 

Lakini jeshi la nchi hiyo likiongozwa na wanajeshi vijana lilifanya mapinduzi na kumfanya kuwa kiongozi wa Ghana, Desemba 31, 1981, lilimpomtoa gerezani na  baadaye akaanzisha chama cha National Democratic Congress (NDC), na hatimaye kuwa rais wa nne wa Ghana tangu ilipopata uhuru mwaka 1957.

 

Rawlings amefariki zikiwa zimebaki siku zisizozidi mwezi mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais mwaka huu, 2020.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top