} });
 

 

RAIS wa Marekani ambaye pia alikuwa anatetea kiti chake kwa tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump kwa mara ya kwanza amekiri kuwa mpinzani wake, Joe Biden ameshinda uchaguzi huo uliofanyika Novemba 3, 2020 licha ya hapo awali kuyakataa matokeo na kutangaza kwenda kuyapinga mahakamani.

 

Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema; “Ameshinda uchaguzi kwa kuwa mchakato wa uchaguzi ulikuwa wa wizi,” lakini baada ya dakika chache alisema hamaanishi kuwa alishindwa uchaguzi huo.

 

Trump alirudia tena madai yake ya kuibiwa katika uchaguzi. Alifungua kesi kuhusu madai yake lakini hakutoa ushaidi wowote wa madai yake ya kuibiwa. Mashtaka yake yote yamepuuziwa.

 

Ijumaa iliyopita, maofisa wa uchaguzi walisema uchaguzi ulifanyika katika usalama zaidi katika historia ya Marekani na hakuna ushaidi kuwa kura zilipotea au kuibiwa au kuwa na tatizo lolote la kufanya uchaguzi kutiliwa shaka. Pamoja na ufafanuzi huo , Trump hakukubali kuwa Biden alishinda uchaguzi mpaka sasa.

Ijumaa, msemaji wa Ikulu Kayleigh McEnany aliiambia Fox News: “Rais Trump anaamini kuwa atakuwa rais kwa muhula wa pili.” Katika kutano na wanahabari siku hiyohiyo , Bwana Trump alisema “Nani anajua” mamlaka ipi itakuwa madarakani siku zijazo.

 

Licha ya kukubali ushindi wa Biden katika ujumbe mmoja wa tweet Jumapili hii, rais aliongeza kusema “Sikubaliani na LOLOTE!”. Twitter iliongeza tahadhari kwa Trump kuhusu madai yake na kusema “Madai ya kuibiwa katika uchaguzi yanapingwa”.

 

Maelfu ya wafuasi wa wa Trump wlaiandamana Washington DC Jumamosi kupinga madai yao kufutwa. Maandamano ya amani yalikumbwa na vurugu majira ya jioni baada ya wafuasi ahao kuanza kufanya fujo. Maofisa walisema watu 20 wameshtakiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kushambulia watu naumiliki wa silaha.

 

Tukio moja la mtu kuchomwa kisu liliripotiwa na polisi wawili kujeruhiwa. Kwa sasa kuna msukumo mkubwa kwa Trump kujiandaa kukabidhi utawala. Wakala wa huduma ya uongozi (GSA)wakala wa serikali wanajukumu la kuanza mchakato wa kuwatambua Biden na makamu wake Kamala Harris kuwa washindi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top