} });
 

LEO ni siku ya nne tangu kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura nchini Marekani baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika Novemba 3, mwaka huu ambapo mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha DemocraticJoe Biden anaongoza katika katika kura maalum maarufu kama ‘electoral vote’.

 

Rais Donald Trump ambaye anagombea kwa muhula wa pili amekilaumu Chama Democratic kuwa kinamwimbia kura na kwamba hatokubaliana na matokea ya kushindwa.

 

Trump ametoa tuhuma hizo bila kuwa na ushahidi wowote, na madai yake yamejikita katika uhalali wa idadi kubwa za kura za awali zilizopigwa kwa njia ya posta ambazo ni zaidi ya zile ambazo zilihusisha watu kwenda kupiga moja kwa moja katika siku ile ya uchaguzi ya Novemba 3.

 

Katika madai yake, Trump amesema atachukua hatua za kisheria ili kusitishwa zoezi la kuhesabu kura kwa kukosa imani na matumaini dhidi ya wafuasi wa Joe Biden ambao wameanza kusherehekea nje ya kituo kikuu cha kuhesabu kura.

 

Kwa upande wake Biden amewataka raia wa Marekani kutulia na kuacha zoezi la kuhesabu kura.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top