} });
 

 

KUANZIA siku ya JumapiliUwanja wa ndege wa Bujumbura, Burundi, umefunguliwa kwa ajili ya ndege zinazofanya safari kimataifa baada ya kufungwa kwa miezi saba kutokana na janga la virusi vya corona.

 

Burundi imekuwa nchi ya mwisho ya Afrika Mashariki kufungua anga yake baada ya Tanzania mwezi MaySudani Kusini mwezi JulaiKenya na Rwanda mwezi Agosti na Uganda mwezi Septemba.

 

Mamlaka ya anga imesema, abiria watakaoingia watahitajika kuwasilisha cheti kinachoonyesha majibu ya vipimo vilivyofanywa saa 72 zilizopita yanayoonyesha kutokuwa na maambukizi ya virusi, kufanyiwa vipimo na kukaa karantini kwa saa 72, kwa gharama zao.

 

Melance Ndayisenga, mkazi wa Jiji la Bujumbura, amefurahishwa na kufunguliwa kwa uwanja wa ndege lakini amesema sekta ya utalii imeporomoka kutokana na kufungwa kwa uwanja huo wa ndege. Burundi mpaka sasa imerekodi maambukizi kwa watu 421 na kifo cha mtu mmoja.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top