} });
 

 

Leo November 25, 2020 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema chama hicho hakijatoa majina ya Wabunge wowote hivyo kitaitisha kamati kuu na kutoa maamuzi.

“Kwa kuwa jambo hili ni la dharura natangaza wito (Public notice), kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana, kufika makao makuu ya chama bila kukosa siku ya Ijumaaa ya Novemba 27, 2020, saa 2:00 asubuhi” John Mnyika

“Kutoka popote pale walipo kamati kuu inaweza kuchukua hatua za dharura kama itaona maslahi ya jumla ya chama yanaweza kuathiriwa” John Mnyika.

“Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote ya mtu yeyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kujazwa na kiapo cha hakimu kwahiyo kwa tafsiri nyepesi ni kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi, wameenda kuapishwa bila baraka ya chama” John Mnyika

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top