} });
 


RAIS  John Magufuli amewaondoa hofu wakuu wa mikoa na wilaya ambao wamekuwa wakimpigia simu na kumwandikia meseji wakijieleza kuwa katika vipindi vyao wamefanya kazi vizuri hivyo wangependa waendelee kufanya naye kazi katika awamu yake hii ya pili.

 

Amesema hayo leo Jumatatu, Novemba 9, 2020, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati akihutubia baada ya kumaliza kumwapisha mwanasheria mkuu wa serikali, Profesa Adelardus Kilangi na kuwaeleza wakuu hao wa mikoa na wilaya kutokuwa na hofu badala yake wakachape kazi.

 

“Pamekuwa na tabia kila serikali mpya inapoingia au awamu mpya inapoingia, watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya serikali, kwamba yanatokea mabadiliko na sasa hivi naona wenye hofu sana ni wakuu wa mikoa na wilaya na nawashangaa kwa nini wanakuwa na hofu.

 

“Kama ni mafanikio ya serikali ni pamoja na wao, kama ni ushindi wa asilimia 84 ni pamoja na wao wamewezesha ushindi huu kupatikana kwa kufanya kazi nzuri. RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama performance yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba mheshimiwa rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa.

 

“Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko hata moja, labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo sana, serikali ni ileile, kama nilikuteua uwezo si bado ni uleule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao.

 

“Wakijiandaa kwamba wanaondoka wao labda waandike barua, mimi najua nilianza nao nitamaliza nao, ni hivyohivyo kwa watendaji wengine, vyombo vya ulinzi na usalama si ni hivyo hivyo sasa unabadilisha kitu gani wakati wewe ndiyo uliowaweka.

 

“Yaani kila mwaka ukiingia unaanza kuapisha, hata kuapisha kunachosha, nianze tena kuapisha wakuu wa mikoa 26, ma-DAS na wakuu wa wilaya siwezi.  Tumeshamaliza.  Wachape kazi ila atakayejiondoa mwenyewe ndiyo nitaapisha ila AG kafanye kazi. Hakuna mabadiliko, tulianza wote tutamaliza wote, kwa hiyo tukafanye kazi.

 

“Mabadiliko yatakuwa kwa mawaziri kwa sababu tulikwenda kuomba kwa wananchi wengine wamerudi wengine hawakurudi, lakini tunao wabunge 264, hivyo tuna nafasi kubwa ya kuchagua, hilo lazima niwaambie ukweli. Baada ya hapo twende tukachape kazi pamoja,” amesema Magufuli.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top