} });
 

MBUNGE wa Jimbo la Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, amekutana na kigingi cha kwanza bungeni wakati akiomba kura za wabunge ili wamchague kuwa Spika wa Bunge la Tanzania kwa kipindi cha pili (2020-2025).  

 

Ndugai aliwahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 na  Spika wa Bunge la 11, .

 

Katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dodoma, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai, alimteua mbunge mteule wa Isimani (CCM), William Lukuvi, kuwa mwenyekiti wa uchaguzi wa Spika wa Bunge la 12 ambao ameuendesha vizuri. 

 

Akizungumza wakati wa kuomba kura, Ndugai amesema: “Mkinipa nafasi hii nitasimamia katiba yetu na kutenda haki kwa wabunge wote, nitalifanya Bunge la 12 kuwa la mfano.  Haijawahi kutokea tangu Uhuru. Wabunge waliotoka upinzani tutawalinda na hakutakuwa na tofauti hivyo naomba kura zenu ili kupata nafasi hii ya Uspika.

 

“Upande wa upinzani, hatutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuwa hawatatimiza asilimia 12, uongozi wa spika, ofisi ya Bunge tutawatendea haki kabisa.”

 

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani (CHADEMA) akimuuliza swali mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge Tanzania, Job Ndugai wakati wa mchakato kwa uchaguzi wa spika amesema:

 

“Wewe ulikuwa Spika Bunge lililopita, kama mwanadamu una mapungufu. Je, unategemea kuonyesha kipi cha tofauti katiba Bunge hili kutokana na mapungufu machache uliyokuwa nayo kwa Bunge lililopita?”

 

Kwa upande wake, Ndugai alijibu: “Kwanza nianze kwa kumpongeza Aida Khenani, maana amemshinda rafiki yangu Ally Keissy. Na alikuwa anasema hapa ‘tutakutana jimboni’ ni kweli wamekutana jimboni.

 

“Kwa hiyo hongera sana. Nimhakikishie tu, na nilisema katika maelezo yangu, wabunge wa upande wa upinzani, maana hatutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa sababu hawajatimiza 12.5% kwa kanuni zetu, nimhakikishie kwamba uongozi; yaani spika na wasaidizi wake wote na ofisi ya bunge; itawatendea haki kabisa kabisa.

 

“Lakini niwahakikishie wabunge wa CCM ambao ni wengi hapa, watawatendea haki kabisa. Na Bunge hili lina wabunge vijana, na wabunge wa upinzani walio wengi karibu wote, isipokuwa wawili watatu, watakuwa ni akina mama — wasichana; na wabunge wengi vijana wako hapa. Watawatendea haki kabisa kabisa, wasiwe na wasiwasi.”

 

Hata hivyo, baada ya kura kupigwa, Ndugai amechaguliwa na wabunge kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili baada ya kupata kura 344 kati ya wapiga kura 345 sawa na asilimia 99.7.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top