} });
 


Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza inawashikilia wahamiaji haramu 52 raia wa Ethiopia waliokuwa wamejificha kwenye nyumba ya kulala wageni Mabatini na Bukuku kata ya Buhongwa katika Manispaa ya Nyamagana baada ya kuingia nchini Kinyume cha sheria.

Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Bahati Mwaifuge amesema kwa mwezi November pekee yake wamekamata Wahamiaji haramu (59) wote wakiwa Raia wa Ethiopia

“Tulikamata wahamiaji haramu raia wa Ethiopia (52) hawa waliingia makundi mawili kundi la kwanza wanne tulikuwakuta eneo la Mabatini katika nyumba ya kulala wageni, kundi la pili (48) tumewakuta mtaa wa Bugugu kata ya Buhongwa wamehifadhiwa katika nyumba wakijisaidia kwenye mabeseni”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top