} });
 

 

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, amewasimamisha kazi maofisa 8 wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro kwa madai ya kujihusisha na rushwa pamoja na kuisababishia serikali hasara.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa RC Shigella, kuwa vitendo vya rushwa vimekithiri katika ofisi za watumishi wa serikali katika boda hiyo, na ndipo alipoamua kuunda kamati maalumu ya uchunguzi iliyoanza kazi yake Novemba 18 kwajili ya kuchunguza mwenendo wa watumishi hao.

“Hapa wamegeuza kuwa ni shamba la bibi, hawa wanaenda kwenye taratibu za kiuchunguzi na vyombo vya dola viwachukue wakaanze kutoa maelezo kwanini wasipelekwe mahakamani, na hapa waletwe watumishi wengine tunataka kituo cha Horohoro kiwe cha mfano kwa kuhudumia wateja” RC Shigella

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top