} });
 

 

Na Magdalena Kashindye

Baadhi ya wananchi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamelalamikia huduma na lugha mbovu zinazotolewa katika hospitali ya mji wa kahama hususani wakati wa usiku kwa kutozwa bei kubwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kahama baba wa mtoto aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo kwa upungufu wa damu Maximiliani Donald amesema alimfikisha mtoto wake hospitalini hapo akaambiwa anaupungufu wa damu na anapaswa kuleta watu watatu wa kutoa damu. 

Maximiliani amesema aliwaomba wahudumu atoe damu moja ili mtoto wake aweze kuhudumiwa kwa usiku huo na asubuhi ndipo alete watu wengine wawili wa kutoa damu mbili ambazo zitabaki kwenye benki ya damu lakini alikataliwa na kupelekea mtoto wake kukaa bila kuhudumiwa hadi majira ya saa tano usiku walipotafuta msaada zaidi. 

Naye Donald Lucas amesema kuna ubadhilifu kwenye duka la dawa lililopo dani ya hospitali hiyo kwani usiku waliandikiwa kwenda kununua mirija ya kutolea damu waliuziwa mrija mmoja kwa shilingi elfu 29,500 na walishindwa kumudu gharama hiyo ya kununua mirija mitatu na kulipokucha wahudumu wa hospitali hiyo waliwataka wakanunue miraji hiyo kwenye duka hilo kwa kuwa bei ya shilingi elfu 29,500 ilikuwa ni ya usiku na bei ya mchana ni shilingi elfu 5,000. 

Kwa upande wake mgaga mfawidhi wa hosipitali ya mji wa Kahama Dr. George Masasi amesema kilichotokea ni kutoelewana kwa lugha kati ya muhudumu na wauguzaji lakini utaratibu unaotakiwa ni kutoa damu moja unalipa mbili kutokana na wakazi wengi wa Kahama kuwa na magonjwa ya kuambukiza. 

Aidha Mkurugenzi mtendaji wa mji wa Kahama Bw. Anderson Msumba amesema hakuna bei ya mchana na usiku na tayari amechukua hataua za kinidhamu kwa baadhi ya watumishi na wamefikishwa TAKUKURU kwa uchunguzi zaidi.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top