
BAADA ya Wabunge wenzao 4 kufukuzwa kazi, Wapinzani wote 15 ambao ni watetezi wa demokrasia wamejiuzulu ikiwa ni ishara ya kuonesha mshikamano wa kupinga kutimuliwa kwa wenzao, Hong Kong, China.
Serikali ambayo ipo Beijing imepitisha Sheria inayoruhusu Mamlaka ya Jiji hilo kuwafukuza kazi Wanasiasa ambao wanaonekana kuwa tishio kwa usalama wa Taifa.
Chini ya Sheria hiyo Serikali ina mamlaka ya kuwaondoa wabunge moja kwa moja bila kwenda mahakamani.
Hatua hiyo inatajwa kama hatua nyingine ya China kudhibiti Uhuru wa Hong Kong, jambo ambalo linapingwa vikali Hong Kong inakataa.
Wakazi wa Hong kong mara kwa mara wameingia kwenye mzozo na polisi kutokana na maandamano yasioisha yakishinikiza kujitenga na China.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment