} });
 

 

POLISI mkoani Morogoro inawashikilia wafanyabiashara wawili wanaofahamika kwa majina ya Husein Sadick Juma (29) mkazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam na Theresphory  Hamisi (40) wakiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakisafirisha viroba 15 vya bangi yenye uzito wa kilogramu 237 kwa kutumia gari aina ya Toyota Prado namba T168 BWB wakitokea Kijiji cha BonyeMorogoro Vijijini kuelekea Jijini Dar, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

 

Akizungumza na wanahabari mjini Morogoro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Mwanadamizi wa Polisi, SACP Wilbroad Mutafungwa,  amesema mmoja wa watuhumiwa hao alikuwa amevalia sare za JWTZ ili wasisimamishwe na maofisa wa usalama barabarani.

“Dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Husein Sadick Juma alikutwa amevalia kofia na flana ya JWTZ, tulipomuhoji kiundani zaidi tukabaini hakuwa  askari,” alisema Mutafungwa.

 

Aidha, amesema kuwa watuhumiwa wote wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya kusafirisha bangi huku akisema kuwa taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea na muda wowote watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

 

“Tunaendelea kufanya upelelezi kubaini mzigo walikuwa wakiupeleka wapi, na tayari timu yetu imeshafika Dar es Salaam kuendelea na upelezi na kubaini mmiliki wa gari hilo na namna alivyoruhusu gari lake kuhusika kubeba bangi hizo,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top