} });
 


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt. Bashiru Ally  amewakaribisha wanawake kutoka vyama vya upinzania kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa milango iko wazi kupokea wanawake wapambanaji na wenye nia ya kulitumikia taifa.

  

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo Novemba 29, 2020 jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushahidi.

 

“Upinzani walikuwa na wakina Mama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni CCM milango iko wazi”, amesema Dkt. Bashiru. 

 

Akizungumzia suala la ushindi wa Chama, “Hatuna mitambo ya kuiba Kura sisi kama Marekani, sisi mitambo yetu ni mabalozi wetu ambao walifanya kazi Usiku na mchana sababu tulikuwa tunashindana na vyama vilivyoishiwa sera. Vyama vimeshindwa kwa halali vinatafuta sababu kuna Watu wametukana siku 60 za kampeni badala ya kumwaga sera, niwapongeze sana Vijana wa Chama cha Mapinduzi mmeonesha uvumilivu sana kipindi chote cha kampeni”


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top