} });
 


SERIKALI imesema itawachukulia hatua kali za kisheria, ikiwemo kuwanyang’anya leseni wale wote watakaobainika kuuza saruji kwa bei ya juu.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, mara baada ya kutembelea viwanda vya saruji vilivyopo jijini Tanga na kukuta uzalishaji ukiendelea.


Amesema bei ya kiwandani ni kati ya shilingi  10,600 kwa mkoa wa Tanga na nje ya mkoa ni shilingi 11,600 kwa mfuko moja.


Aidha amesema kutokana na kutokuwepo kwa ongezeko la bei kutoka viwandani ya bei ya saruji itabaki kama ilivyokuwa awali na si vinginevyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top