} });
 

 

Petro Mlongo (29), Masumbuko Sakumi (25) na Jackson Masumbuko (26) wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia kwenye kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Walitumia panga kumjeruhi kichwani na mgongoni Zwiyo Mpemba huku wakimpora Tsh. 300,000 pamoja na simu mbili ambazo zote zina thamani Tsh. 120,000.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita, Sosthenes Kiiza amesema adhabu kali imetolewa kwa watatu hao kama fundisho kwa wengine wenye tabia za ukatili wa aina hiyo.

Watatu hao wameomba kupunguziwa adhabu wakisema wazazi wanawategemea lakini Hakimu Kiiza ametupilia mbali utetezi wao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top