} });
 

 

Kamati ya utendaji ya Yanga SC imemsimamisha kazi kaimu katibu mkuu wao na Mkurugenzi wa sheria na wanachama wakili Patrick Simon ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Bado haijawekwa wazi moja kwa moja ni tuhuma zipi hasa zinamkabili wakili Patrick lakini Inaaminika kuwa ni miongoni mwa zile zinazotolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mwinyi Zahera.

Hivi karibuni video ya Zahera ilisambaa na kumtuhumu kuwa wakili Patrick amekuwa akitoa majibu sio mazuri kwa FIFA kitu ambacho kinaweza kuigharimu Yanga, inasemekana Zahera bado anaidai Yanga na kesi iko FIFA.soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top