} });
 


Mwenyekiti Chadema Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na wajumbe watatu wa kamati kuu wameripoti kituo cha polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Jumatatu Novemba 09

 

Wengine ni aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Chadema) Halima Mdee na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini Godbless Lema.

 

Mbowe, Lema na Jacob walikamatwa na polisi Novemba Mosi, 2020 huku Zitto akikamatwa Novemba 03, 2020 katika kituo cha polisi Oysterbay alikokwenda kuwajulia hali wenzake. Wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti leo.

 

Mdee alijisalimisha polisi jana baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumtaka kuripoti kwa mahojiano.

 

Leo (jana) viongozi hao waliwasili kituoni hapo kwa nyakati tofauti na kuelekea kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi na ilipofika saa 4:30 walitoka kwa pamoja.

 

Hata hivyo, baada ya kutoka Mbowe hakutaka kuzungumza chochote badala yake aliagana na Zitto akieleza anarudi kituoni kwa ajili ya kufuatilia wafuasi wa chama hicho wanaoendelea kushikiliwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top