} });
 

 

HABARI ni kwamba, Kocha wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge ambaye alihusika kwenye dili za wachezaji Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe kutua Yanga, anatajwa kuwa yuko mbioni kulishusha jembe jipya ndani ya kikosi hicho.

 

Jembe jipya ambalo linaletwa na Ibenge ni straika Dark Kadima Kabangu anayeitumikia DC Motema Pembe ya nchini humo.


Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, hadi sasa kuna matumaini makubwa ya Kabangu kutua Jangwani, kutokana na Ibenge kuhusishwa katika dili hilo.“Tunaendelea kumshukuru Mungu, hasa katika mipango yetu ya usajili wa dirisha hili dogo, ambapo karibia kila mchezaji tuliyemhitaji tunaona kabisa mambo yetu yanaenda kufanikiwa, zaidi tunafurahishwa na wadau wanaotufanyia dili hizi hususan kocha Ibenge.“

 

Kama hakutakuwa na mabadiliko ya aina yoyote katika makubaliano yetu na Klabu ya Motema Pembe, ni dhahiri kabisa safu yetu ya ushambuliaji inaenda kuwa hatari zaidi kwa kutua Kabangu,”


Kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni, Kabangu alisema: “Ni kweli Yanga wameshazungumza na uongozi wangu, hivyo nasubiri wakamilishe tu dili kisha nione namna ya kufanya uhamisho wa kuja Tanzania.”


Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, ameibuka na kubainisha kwamba, anasaka majembe mawili tu kuimarisha kikosi chake.“Kuhusu suala la usajili kwa sasa nafi kiria tumalize hesabu mapema tu kwa ajili ya kuendelea na masuala mengine ya timu hasa kwenye ligi.“

 

Kwa sasa nataka kusajili wachezaji wawili pekee ambao watakuja kuongeza nguvu kwenye timu ambao watakuwa na tofauti na kuongeza kitu kwa hawa waliopo,” alimaliza Kaze.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top