} });
 

 

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Getrude Ngoma (26) wa mjini Ndola nchini Zambia, amempeleka mchumba wake mahakamani kwa kushindwa kumuoa baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa muda wa miaka nane tena akiwa amemzalisha mtoto.

Getrude amesema amechoka kumvumilia mwanaume huyo aliyefahamika kwa majina ya Herbert Salaliki ambaye alimuahidi kumuoa na badala yake hajafanya hivyo kwa kisingizio cha kutomudu gharama za harusi wakati tayari amekwisha toa mahari.

Jaji Evelyn Nalwize ambaye ameisikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Jimbo la Kabushi, Ndola alimshauri Getrude kumaliza madai ya tofauti zao nje ya mahakama.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top