} });
 

Akiwa chini ya jeshi la polisi baada ya kusomewa mashta yake.
 

Mfanyabiashra mkazi wa Kinondoni Bwawani jijini Dar es Salaam,  Benedict Kimbusu, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka kusambaza maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, Adolph Ulaya, mbele ya Hakimu Mfawidhi Yusto Ruboroga imedai kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo, kati ya Februari 27, 2014 na Desemba 7 mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam.


Inadaiwa mshtakiwa alisambaza maudhui kupitia Chanel ya YouTube iitwayo Pioh the 9os Lyrics bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka ya mawasiliano TCRA.


Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ametakiwa kuwa na wadhamini watakaosaini bondi  ya sh. Milioni tatu. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 30, mwaka huu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top