} });
 

 

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limempiga faini ya USD 10,000 (Tsh milioni 23.1) nahodha wa Arsenal na timu ya taifa ya Gabon Pierre Emerick-Aubameyang kwa kosa la kupost picha inayoishushia hadhi CAF wakati Gabon walipokuwa wamekwama Airport Gambia kwa madai ya kucheleweshwa kwa makusudi na wenyeji wao kama njia ya kuwatoa mchezoni.

Pamoja na hilo Gambia nao wamepigwa faini ya USD 100,000 (Tsh milioni 231.8) na onyo ya kutotenda kosa kama hilo kwa kipindi cha miezi 24 la kutowaandalia mapokezi mazuri wageni wao.

Gambia hawakuwapokea vizuri Gabon wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 ambapo mwisho wa mchezo Gambia walishinda 2-1.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top