} });
 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linamsaka baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Nyamasula Sangesange (43), mkazi wa Songambele Kata ya Nyanguku Wilaya ya Geita kwa tuhuma za kumshambulia mwanaye.

 

Jeshi hilo linamtafuta baba huyo kwa kumkatakata kwa mapanga mwanaye sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na kumkata vidole vitatu.

 

Baba huyo anadaiwa kumfanyia unyama huo mwanaye huyo aliyefahamika kwa jina la Jumanne Msolwa (22) baada ya kumtuhumua kuwa ameuza kuku wake.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Henry Mwaibambe alieleza;

“Ilikuwa saa mbili usiku, huyu baba alimshambulia mtoto wake kwa mapanga.

 

“Kiini cha tukio hili ni kwamba kijana huyu ni mjasiriamali mdogomdogo.


“Sasa pale kwa baba yake anafuga kuku na ana ng’ombe wawili. Pia ana bustani, sasa aliamua kuuza kuku wake mwenyewe ili waweze kumsaidia kuendeleza bustani yake.

 

“Baada ya kijana huyu kuuza kuku wake, sasa baba akawa amechukia, akaamua kumshambulia mtoto wake kwa mali ya kwake mwenyewe.


“Kijana huyu aliumizwa sana, akafikishwa hospitalini kwa matibabu.”

 

Kufuatia tukio hilo na matukio mengine ya aina hiyo katika Mkoa wa Geita, kamanda huyo alisema kuwa, Jeshi la Polisi linaendelea kumfuatilia mtuhumiwa huyo na litahakikisha sheria inafuata mkondo wake.


Pia alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kudhibiti vitendo vya uharifu vinavyotokea mwishoni mwa mwaka.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top