} });
 

 

Chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba Newala (TANECU) kimefanikiwa kuuza korosho tani elfu moja na miatisa na ishirini na tano zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu na milioni mianne katika mnada wa kumi na mbili huku wakulima wachache waliohudhuria wakilalamikia kushuka kwa bei ya zao hilo kunavyowaadhiri kimapato.

Akizungumza katika mnada uliyoendeshwa kwa njia ya sanduku na mtandao meneja wa chama kikuu cha ushirika (TANECU) Mohammed Nasoro  amesema bei ya juu ya korosho gha kilomoja katika mnada huo ni shilingi elfu mbili na miamoja na sitini na saba, wakati bei ya chini korosho daraja la pili zimeuzwa kwa shilingi elfu moja miasita sabini hadi elfu moja na miatano ishirini na tano.

Hata hivyo amesema wakulima wameridhia kuuza kwa bei hiyo kutokana na kila mnada bei ya zao hilo kuendelea kushuka na kusisitiza kuwa korosho zote zilizokuwa kwenye maghala ya Tandaimba na Newala zimeuzwa.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Newala na Tandaimba wameiomba serikali kuingilia kati bei ya zao hilo ambalo kila mnada zimeendelea kushuka na hivyo kutomnufaisha mkulima.

Mnada wa kumi na tatu unatarajiwa kufanyika Alhamisi ijayo katika halmashauri ya wilaya ya Tandaimba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top