} });
 

 

Imeelezwa kuwa nyota wa kikosi cha Namungo FC inayoshiriki Kombe la Afrika ikiwa imepenya hatua ya mchujo, Shiza Kichuya amefungiwa kuendelea kutumika ndani ya kikosi hicho kwa miezi sita.

 

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo wa zamani wa Simba alisajiliwa na timu hiyo akiwa na mkataba na Klabu ya Pharco ya Misri.

 

Alijiunga na Klabu hiyo msimu wa 2018 akitokea ndani ya Simba na alisepa kimyakimya kutokana na kukosa namba ya kudumu kikosi cha Kwanza ambapo alicheza jumla ya mechi 3 pekee.

 

Alirejea Simba msimu wa 2019/20 ambapo alisaini dili la miezi sita hivyo kwa kosa hilo inaelezwa kuwa Simba imepigwa faini na FIFA.

 

Simba wameepuka adhabu ya kufunguliwa usajili lakini watalipa faini ya dola 130,000, zaidi ya Sh milion 300.

 

Habari kutoka chanzo cha ndani ya Namungo imesema kuwa taarifa hizo zipo mezani hivyo wanazifuatilia ili kujua hatma yao itakuaje.

KUSAMBARATISHA MIKATABA YA KISHETANI by MTU WA MUNGU VINCENT

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top