} });
 

 

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia watu watatu kwa kosa la mauaji ya mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Celestina Manyanda (70), mkazi wa kijiji na Kata ya Nyaluyeye Tarafa ya Busanda wilayani Geita.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Henry Mwaibambe anasema kuwa, sababu za mauaji ya mama huyo ni mgogoro wa ardhi eneo la uchimbaji wa madini.

 

Kamanda huyo anasema kuwa, siku ya tukio hilo, watuhumiwa hao walifika nyumbani kwa marehemu muda wa saa mbili usiku na kuanza kumshambulia maeneo ya kichwani, shingoni na mgongoni kwa kutumia kifaa chenye ncha kali ‘moko’ wakati akitoka ndani kwenda kuoga.

 

“Marehemu Celestina aliamka kwenda kuoga ndipo akakutana na watu hawa waliomshambulia na kupoteza maisha papo hapo. Ugomvi huu ni wa kifamilia, hawa watuhumiwa ni ndugu zake na inaelezwa kuwa wana ugomvi mkubwa wa namna ya kugawana eneo la kuchimba madini.

 

“Huyu mwanamke mume wake ana umri wa miaka 90, walikuwa wanaishi wote, lakini nadhani hawa wauaji walitumia nafasi hii kwa kuona hawa watu wote ni wazee, hawana uwezo wa kujiokoa,” anasema.

 

Kamanda huyo anaongeza kuwa, watuhumiwa hao walimtuhumu mama huyo kuwa anataka kujimilikisha eneo kubwa la kuchimba madini ndipo walipoamua kujichukulia sheria mkononi.

 

Hata hivyo, anasema kuwa, watuhumiwa hao walitambuliwa na sasa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa jili ya taratibu zaidi za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top