} });
 


KAULI aliyoitoa kiungo fundi wa Plateau United ya Nigeria, Isah Ndala akisema amekubali kutua Yanga endapo klabu hiyo itafuata taratibu zote za kumsajili katika dirisha hili dogo la usajili, inaweza kuleta matumaini makubwa kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.

 

Kiungo huyo ameongeza kwamba, tayari ameshafanya mazungumzo na Yanga, anachosubiri ni kukamilisha mambo kadhaa kabla ya kuanza kuitumikia timu hiyo.

 

Ndala alionekana kuwavutia mashabiki wengi wa soka hapa nchini mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba uliofanyika wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar na kumalizika kwa suluhu.

 

Kiungo huyo aliwavuruga vilivyo viungo wa Simba wakiongozwa na Jonas Mkude na kuonekana kulitawala eneo hilo ingawa hakuisaidia timu yake kusonga mbele.

 

Akizungumza moja kwa moja kutoka Nigeria, Ndala alisema: “Nimefanya mazungumzo na Yanga ambao wameonyesha nia ya kunihitaji kunisajili, mimi nipo tayari kujiunga na Yanga iwapo watafuata taratibu zote za usajili kwani mpira ni sehemu ya maisha yangu na kama wataleta dili zuri basi nitafanya nao kazi.“

 

Kuhusu mkataba wangu na Plateau huu ni msimu wangu wa mwisho, hivyo wakati uliobaki naruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote ile juu ya usajili wangu.”


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top