} });
 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama.

POLISI Mkoa wa Kigoma limesema kuku aliyezaliwa na  mwanamke mkoani humo, atapelekwa kwenye Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya kuchunguzwa kwani si kawaida kwa binadamu kujifungua kiumbe cha namna ile.

 

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama, leo Desemba 72020, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, na kusema kuwa tukio la mwanamke huyo kujifungua kuku lilitokea  Desemba 5, 2020, katika kituo cha afya Uvinza.

 

“Kwa kuwa tukio hili siyo la kawaida kwenye jamii, jeshi la polisi tutachukua kiumbe hicho kwa ajili ya kupeleka Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani siyo kawaida kwa binadamu kujifungua kuku”, amesema  Manyama.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top