} });
 


Kutoka Kagera tumeamka na hii taarifa ya moto kuunguza maduka zaidi ya 10 na kuteketeza baadhi ya vitu katika majengo yanayomilikiwa na Familia ya Nekemia Kazimoto (Kazikomu) yaliyopo Mji wa kayanga mjini, Karagwe, mkabara na majengo ya city center na Magereza ya kayanga.

Moto huo umeibuka usiku wa kuamkia leo katika moja ya duka la nguo na kusambaa katika maduka mengine ya bidhaa za vyakula, hoteli, stoo za vifaa vya ujenzi, saloon na maduka ya bidhaa mchanganyiko, moto umedumu kwa zaidi masaa manne na chanzo cha moto hakijafahamika mpaka sasa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top