} });
 

SERIKALI a imeruhusu ufungwaji wa magari yanayotumia nyaya angani (cable cars) katika Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika ili kuchochea utalii.

 

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari waandamizi jijini DodomaKamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA, Paul Banga, amesema erikali imeipa TANAPA ruhusa ya kuwekeza katika kufungwa kwa magari hayo.

 

“Tunasubiria maelekezo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kabla hatujaanza kutafuta mwekezaji kwa ajili ya mradi huo,” amesema Banga.

 

Aidha, amesema kufungwa kwa ‘cable cars’ kwenye milima si kitu kigeni, huku akiwatoa hofu waongoza watalii kwamba shughuli za kupanda mlima kwa kutembea zitaendelea.

 

Amesema usafiri huo utawasaidiza zaidi walemavu na watu wenye matatizo ya kiafya ambao hawawezi kitembea umbali mrefu kupanda mlima huo.

 

Amefafana kwamba magari hayo yatawekwa hadi umbali wa mita 3,700 kati ya mita 5,895 za mlima huo kutoka usawa wa bahari.

 

Takribani watalii 50,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani hupanda mlima huo kwa mwaka, hata hivyo si wote wanaofanikiwa kufika katika Kilele cha Uhuru.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top