} });
 


Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Mafisadi, imeahirisha kutoa hukumu katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara maarufu nchini, Ayubu Kiboko na mkewe Pilly Mohamed hadi Desemba 18,mwaka huu.

 

Uamuzi huo wa ahirishi umetolewa na msajili wa mahakama hiyo, David Ngunyale baada ya watuhumiwa hao kufikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu yao iliyotarajiwa kutolewa leo.

 

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka uliita mashahidi 16, wakati washitakiwa walijitetea wenyewe bila kuleta mashahidi.

 

Katika Kesi ya msingi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa kukamatwa Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wakiwa wanasafirisha dawa za kuÄşevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 251.25 kinyume na sheria.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top