} });
 

Baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani Kisutu.

WALIOKUWA watumishi  13  Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka sita likuwemo kuharibu noti 460,000 za 10, 000 na kuisababishia benki hiyo hasara ya zaidi ya bilioni 4.6.


Watumishi hao wa BOT ni Mariagoretha Kuzugala, Henry Mbowe, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanakheir Omary.Wengine ni Alistides Genand, Shukuru Mchegage, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Ishengoma ambao walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya.


Wamesomewa mashitaka yao na jopo la mawakili wanne wa serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, ambapo amedai kuwa kati ya Januari mwaka 2017 hadi Septemba 30 mwaka 2019, watu hao kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu.


Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa, katika tarehe hizo na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, washitakiwa  Genand, Mchegage, Chengula,  Chihipo na Ishengoma wakiwa si watumishi wa BoT, kwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kwa makusudi, waliwezesha kutendeka kosa la uhalifu wa kulipanga.


Katika shitaka la tatu, imedaiwa kwamba, katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo wote waliharibu noti kwa kukata noti 460,000 za 10,000 sawa na Sh bilioni 4.6.


Mawakili hao wa serikali waliendelea kudai kuwa katika tarehe na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, kwa mawasilisho ya kilaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli washitakiwa wote walijipatia faida ya sh bilioni 1.533 kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo BoT.


Katika shitaka la tano la utakatishaji fedha ilidaiwa kuwa watumishi hao wa BoT  na wenzao hao walijihusisha katika miamala tofauti ya sh. Bilioni 1.533 wakati wakijua zilitokana na kosa tangulizi la uhalifu wa kupangwa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Katika shitaka la mwisho, washitakiwa wote katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, waliisababishia BoT hasara ya sh Bilioni 4.6.


Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa hao walielezwa kwamba, mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi hivyo walipelekwa mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika.


Wakili Kadushi amedai, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamlika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo imepangwa Desemba 28 mwaka huu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top