} });
 


UONGOZI wa timu ya FC Platinum ya nchini, Zimbabwe umeweka wazi kuwa watakuwa na kazi kubwa katika mchezo wa marudiano na Simba kutokana na wapinzani wao kucheza mbele ya mashabiki.

 

Platinum na Simba zitakutana katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba itaanzia ugenini katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kati ya Desemba 22-23, kabla ta mchezo wa marudiano utakaochezwa Januari 4-5, mwaka huu.

 

Msemaji wa FC Platinum, Chido Chizondo, ameliambia Championi Jumatatu wanatamani kuona wanapata nafasi ya kucheza mchezo huo mbele ya mashabiki wao lakini haitawezekana kutokana ugonjwa wa Corona hali ambayo wanaamini itawabeba Simba katika mchezo wa marudiano.

 

“Tulipenda kuona mchezo wetu na Simba tucheze mbele ya mashabiki wetu wakiwa wamefurika uwanjani, naamini ingekuwa na msaada mkubwa bahati mbaya haitowezekana.

 

“Mipango yetu kwa sasa ipo katika mechi ya ugenini kwa sababu tutacheza mbele ya mashabiki wa Simba kutokana na suala la Corona kwao halipo kama kwetu, tunajaribu kuweka wachezaji katika mazingira mazuri ya kisaikolojia ili kwetu isije ikatupa tabu ugenini lakini kuhusu mikakati na mipango katika mechi ya nyumbani ipo vizuri,” alisema Chizondo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top