} });
 

 

WAKATI dirisha dogo la usajili Tanzania Bara likikaribia, si ajabu kwa majembe matatu ya Plateau United kutua Simba baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji, kuondoka na majina matatu ya nyota wa kikosi hicho.

 

Sven amechukua majina ya nyota hao baada ya kukoshwa na kiwango chao wakati walipocheza nao Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Nyota wa Plateau ambao Sven amechukua majina yao ni beki wa kati Ikefe Andrew aliyevaa jezi namba 20 aliyekuwa na rasta, kiungo mkabaji Isah Ndaca aliyevaa namba 17 na Oche Ochewich ambaye alivaa jezi namba 13.

 

Nyota hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Plateau United kilichotoka suluhu Jumamosi dhidi ya Simba kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kocha huyo amesema kwamba wachezaji hao walikuwa wazuri na walicheza kwa kiwango kikubwa katika mechi hiyo na ndiyo ambao walimvutia kwa upande wa Plateau United.

 

“Kuna wachezaji wanne wazuri wa Plateau United walicheza vizuri, yule beki wao namba 20, namba 17 na 13. “Hawa walikuwa wazuri kwa wapinzani wetu na kiukweli hii ni timu nzuri kucheza nayo na wako vizuri sana,” alimaliza Sven.

KUBALI BWANA AYABADILISHE MAISHA YAKO KWA IMANI by MTU WA MUNGU JOVIN MWEMEZI

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top