} });
 


Hali ya kutatanisha imezuka Kasikeu, Makueni nchini Kenya wakati Pasta aliyeitwa kuwakemea mapepo aliposhambuliwa na nyoka katika nyumba ya jirani ya muumini wake.

 

Katika kisa hicho kilichochapishwa kwenye gazeti la Taifa Leo, mwenye nyumba hiyo alimuendea jirani yake kumuomba usaidizi akilalamika kuhusu kusumbuliwa na mapepo.

 

Jamaa huyo alimuahidi kumletea mchungaji aliyesifika katika kuwakemea mapepo na kuwafukuzilia mbali na kumuondolea taabu ya mizimu hao.

 

Pasta huyo aliyeitwa kuwakemea mapepo waliokuwa wakimsumbua bwana huyo kwenye boma lake na hakusita kufika kwa kazi hiyo. Sku ya tukio hilo la kustaajabisha, mchungaji huyo alifika nyumbani humo tayari kuwa kuwakemea mapepo hao.

 

Kabla kuanza maombi, alimuomba jamaa huyo kutoa sadaka ili kumpa Mungu haki yake na kufanikisha shughuli hiyo. Jamaa alitoa KSh 5000 kisha pasta akaanza maombi huku akizunguka kila pande ya nyumba hiyo.

 

Alipofika nyuma ya nyumba hiyo, nyoka wawili walijitokeza ghafla na kuanza kumshambulia mchungaji huyo aliyetimka mbio kujinusuru huku akipiga nduru/kelele.

 

Baada ya pasta kukimbia, inadaiwa kuwa nyoka hao walitoweka kimuijiza na kuwaacha wengi vinywa wazi wengine wakikimbia kwa uoga mwingi.

 

Mwenye nyumba hiyo alilazimika kujifungia ndani ya nyumba yake ishara ya kuogopa huku wenyeji wakidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa majoka hao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top