} });
 


Mchungaji wa Kanisa la Shalom Internation lililopo Sinza jijini Dar es Salaam, Billioneire Mkeu miaka(44) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabikiwa na shtaka la moja la kutoa taarifa za uongo kinyume cha sheria.


Akisomewa hati ya mashtaka na  Wakili wa Serikali Grace Mwanga, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amedai kuwa  katika tarehe tofauti mnamo Februari 2016, katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaama mshtakiwa alitoa taarifa za uongo kwa Ofisa Ardhi, aitwaye Nyendo Kaombwe kuwa yeye ni mmiliki halali wa kiwanja namba 3391, kitalu “A” kilichopo Mbutu  Kigamboni, wakati akijua ni uongo na kufanya hivyo ni Kosa kisheria.


Baada ya kusomewa kosa hilo wakili amesema Upelelezi umekamilika na Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, itakapotajwa.


Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana aliyotakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja akitakiwa kutoka taasisi ya serikali na mwingine taasisi inayotambulika na serikai pia  kuwa na mali isiyohamishika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top