} });
 

 

Mkurugenzi wa kampuni ya Mr. kuku farmer ltd, Tariq Machibya (29), maarufu kama Mr Kuku, aliyekuwa akikabiliwa  na kesi ya kufanya biashara haramu ya upatu  na kukusanya fedha za umma sh. Bilioni 17, amehukumiwa kulipa fidia ya zaidi y sh. Bilioni 5.4 baada ya kukiri mashtaka ya kushiriki katika upatu na kupokea miamala ya fedha kutoka kwa umma.


Mahakama pia imemuhukumu mshtakiwa  kulipa faini ya sh. Milioni tano ama akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.


Aidha mahakama imeamuru fedha sh. 5,456,480.41 ambazo zipo katika akaunti za mshtakiwa zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Godfrey Isaya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amesema mahakama imezingatia kwamba mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa yake na ni mkosaji wa mara ya kwanza na wameangalia makubaliano hivyo hakuna sababu ya kumpa adhabu kali.


Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amedai mshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wameingia makubaliano , katika mashtaka saba aliyokuwa anakabiliwa nayo yameondolewa na wamebakisha mashtaka mawili.


Akisomewa mashtaka hayo mawili, katika shtaka la kusimamia biashara ya upatu inadaiwa  kati ya Januari 2018 na Mei, mwaka huu, maeneo tofauti Dar es Salaam alijihusisha na biashara hiyo kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma kwa kujifanya  watafanya ujasiriamali wa ufugaji kuku na watapata faida asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa uwekezaji wa miezi sita kiasi ambacho ni kikubwa kibiashara kuliko mtaji uliokusanywa.


katika shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa kukubali kupokea muamala wa kifedha kutoka kwa umma kiasi cha Sh bilioni 17.


Awali mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka saba ambapo mbali na hayo mawili  yalikuwepo mashtaka matano ya utakatishaji  fedha.


Kabla ya kusomwa kwa adhabu, Wakili Kadushi aliieleza mahakama kuwa, hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya washitakiwa hivyo, ameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria huku ikizingatia hatua ya makubaliano waliyofikia.

Upande wa wakili wa Utetezi, Augustine Shio ameiomba mahakama impunguzie mshtakiwa adhabu  kwani amekiri makosa yake mwenyewe na pia ana familia ya wake wa watatu ambao kila mmoja anamtoto mchanga na wote wanamtegemea yeye.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

  1. ยินดีต้อนรับสู่ UPLAY365.COM เว็บพนันออนไลน์ All In One ที่รวมเว็บพนันออนไลน์อันดับ 1 ไว้ที่เดียวกันมากที่สุด ไม่ว่าจะเป็น เกมส์ไพ่ ที่เป็นที่นิยม เช่นบาคาร่า แบล็คแจ็ค เสือมังกร หรือจะเป็น รูเล็ต สล็อตออนไลน์ คีโน โป๊กเกอร์ forex ไก่ชน เกมส์ยิงปลา แทงบอล แทงบาส เทนนิส ESPORT แทงมวยไทย และอื่นๆอีกมากมาย พร้อมเทคโนโลยีชั้นนำจากผู้ผลิตซอฟต์แวร์เกมส์ระดับโลก ความน่าเชื่อถือได้มาเป็นอันดับ 1 สามารถเล่นได้ทั้งบนคอมพิวเตอร์ , มือถือ ระบบ android และ IOS *คาสิโนออนไลน์ : สามารถเลือกเล่นกับคาสิโนชั้นนำดังนี้ SexyBaccarat, AG Casino, GOLD Casino, SA Casino, W88 Casino, D88 Casino, WM Casino, GD Casino เป็นต้น *แทงบอล : U กีฬา (U SPORTS) , S กีฬา (S SPORTS) มั่นใจได้เลยว่า อัตราการจ่ายค่าน้ำดีที่สุดต้อง uplay365 เหมาะสำหรับทั้งนักพนันมืออาชีพและ มือใหม่ โดยทางเรามีพนักงานคอยสอนเรื่องการแทงบอลเบื้องต้น แทงง่าย อัตราจ่ายดี *สล็อตออนไลน์ ,เกมส์ยิงปลา : JOKER123,PLAYTECH และอื่นๆ อีกมากมาย ทั้งหมดนี้ สามารถเล่นได้ใน 1 ยูสเซอร์เท่านั้น สนใจสมัครสมาชิกรับเครดิตฟรี สามารถสมัครได้ตนเองที่หน้าเว็บ หรือติดต่อ Callcenter โดย ทางเรามีพนักงานไว้บริการและแก้ปัญหา ตลอด 24 ชั่วโมง สอบถามข้อมูลเพิ่มเติมได้กับแอดมินได้ตลอด 24 ชม.ค่ะ

    GD Casino
    Premium Casino

    ReplyDelete

 
Top