} });
 

 

MTOTO wa prodyuza maarufu hapa nchini anayemiliki studio ya Bongo Record, Paul Matthysse ‘P Funk’, Patricia, amemponza msanii wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ baada ya video zao kusambaa kwenye mitandao wa kijamii wakiwa pamoja.

 

Kusambaa kwa picha na video hizo hususani katika mtandao wa Instagram, kumeibua maswali mengi huku baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya burudani wakimuasa msanii huyo kukaa mbali na mrembo huyo.

 

Video ya Ommy Dimpoz na Patricia ilivuja wakati wakiongozana huku wameshikana mikono kwenda kwenye usiku wa ‘Beuty Legancy’, uliofanyika katika Hotel ya Hayyat jijini Dar.

 

“Ila Ommy bwana amesahau kilichompata mwenzake Diamond! Mondi alijipendekeza sekunde tu na wakati huohuo akafuta picha za Patricia,” alisema shabiki mmoja na kuungwa mkono na wenzie.

 

“Sasa hivi na yeye tena bila woga kamkumbatia kabisa… kuna kitu ambacho anamtafuta Majani, na siku hizi Majani amekuwa mpole naona hawa kina Ommy wanataka kuchezea anga zake,” alisema shabiki mwingine katika mtandao huo.

 

Baada ya watu kumzonga sana Ommy, kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na video hiyo, RISASI Jumatano lilimtafuta Ommy ambapo alifunguka kuwa hakuna chochote kinachoendelea kati yake na Patra.


“Unajua mimi niko GSM, kwenye hii kampuni niko upande wa masoko na yeye Patra, amekuwa kama balozi wa nguo hapohapo GSM.

 

“Sasa wadau walivyotuona tunaingia pale Hayyat, tulikuwa tunatoka kurekodi tangazo lakini watu wakatutafsiri hivyo. Kwa kweli mimi siwezi kufanya lolote kwa Patricia kwanza namuogopa sana Majani kwa kweli, niwaombe watu wawe na amani tu,” alisema Ommy.

 

Kauli hiyo ya utetezi wa Ommy imekuja wiki chache baada ya msanii nguli nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ naye kujichanganya kwa mrembo huyo kwa kuchapisha picha ya Patricia katika ukurasa wake wa Instagram na kuja kuifuta hapo baadaye.

 

Wakati wadau wakiibua maswali kuhusu hatua hiyo ya Mondi, Patricia naye aliibuka na kukanusha madai ya kuwa katika mahusiano ya kimapenzi Mondi.

 

“Kwa kweli Diamond alikuwa anaonyesha tu kunikubali hakuna zaidi ya hapo, tunasalimiana tu, sina mahusiano yoyote na Diamond. Sijawahi kukutana na yeye ana kwa ana, hatuzungumzi kwa kiwango hicho,” alisema.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top