} });
 

 

RAIS  wa Uganda, Yoweri Museveni, ambaye anawania muhula wa sita madarakani, amesema hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa, na hivyo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo.

 

Amesem: “Mniache niendelee kuongoza kwa sababu raia wa Uganda wananihitaji niwepo. Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda. Nataka niwe na uhakika mahali naiacha Uganda.”

 

Ameongeza kuwa, “Huwa nakasirika sana ninaposikia watu wakiniambia niondoke madarakani, lakini huwa najaribu sana kujizuia na kuwa mtulivu. Kama ulishindwa kufanya nilichokuambia, usilete vurugu kwa kuniambia kwamba niondoke madarakani. Wapiga kura ndiyo wanaoamua…”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top