} });
 

 


MWANAFUNZI wa darasa la tatu (3) katika shule ya msingi Uhamila wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Gilison Ngungulu (8) amefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa la GMCL.


Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki muda wa saa moja usiku katika mtaa wa wa Isisi uliopo Tarafa ya Rujewa.

 

Matei alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kunyesha kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ambayo ilipelekea ukuta wa jengo la la kanisa kuanguka wakati mtoto huyo akicheza eneo hilo na watoto wenzake ambao hawakupata madhara yoyote katika tukio hilo.

 

Alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya wilaya ya Mbarali na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

 

Aidha, Kamanda Matei ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuchukua tahadhari kwa watoto wao hasa katika kipindi hichi ambacho mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali kwa kuhakikisha hawachezi maeneo hatarishi.

 

“Ndugu wazazi angalieni watoto wenu kipindi hichi ambacho mvuya zinanyesha katika maeneo yote hatarishi ili wasiweze kupata madhara ”alisema Matei.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top