} });
 


Iran siku ya Jumamosi imemnyonga mwandishi wa blogu na mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Tehran, Ruhollah Zam licha ya mara kadhaa kuomba kupewa msamaha.

Taarifa za kunyongwa kwa Zam zimetolewa na Shirika la Habari la IRNA na kuthibitishwa na wizara ya sheria ya nchi hiyo.

Zam alihukumiwa kifo na mahakama moja mjini Tehran mnamo mwezi Juni kwa makosa ya kuendesha propaganda dhidi ya utawala wa Iran pamoja na kuchochea maandamano ya umma kupitia tovuti yake ya Amad News.

Mwanablogu huyo kwa sehemu kubwa alikosoa kile alichokitaja kuwa udanganyifu katika Uchaguzi wa Rais wa mwaka 2009 uliowezesha Rais wa Zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kuchaguliwa tena.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top