} });
 

 

Waziri wa usalama wa ndani ya nchi wa nchini Malawi , Richard Banda, amesaini nyaraka kwa ajili ya Nabii tajiri na maarufu Shepherd na mke wake, Mary, vimeripoti vyambo vya habari vya Malawi.

Hii inafuatia ombi la mahakama ya nchi jirani ya Afrika Kusini ambako Bushiri na mke wake Mary wanasakwa na mashitaka ya utakasaji wa fedha na ufisadi.

Mahakama ya juu zaidi nchini Malawi iko tayari kuamua kuhusu kukamatwa kwa wawili hao baada ya kuachiliwa huru bila masharti na mahakama ya hakimu mkazi ambayo ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwasababu hapakuwa na ombi rasmi la kumrejesha lililotolewa na Afrika Kusini.

Mahakama itaamua kuhusu kesi hiyo tarehe 22 Disemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily Times newspaper.

Bushiri na mke wake walitoroka kutoka Afrika Kusini mwezi uliopita, baada ya kukaidi sharti la kulipa dhamana ambayo ilikuwa inawazuia kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka kesi yao itakapokamilika.
Mchungaji huyo au Pastor Bushiri wakati huo alisema kuwa maisha yake yamo hatarini iwapo hataondoka nchini humo.

Serikali za Malawi na Afrika Kusini zilikuwa zimetoa taarifa kuhusiana na kutoroka kwao baada ya rais wa Malawi Lazarus Chakwera -ambaye alikuwa ziarani nchini Afrika Kusini- kushutumiwa kusaidia kutoroka kwa mchungaji Bushiri.

Kesi inayomkabili Mchungaji Bushiri Afrika Kusini
Bushiri, na mke wake na watu wengine wawili wanakabiliwa na shutuma za kutakatisha fedha na mashitaka mengine 419.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top