} });
 

Nguzo ya Shirika la Umeme(Tanesco) ikiwa imeanguka eneo la karibu na Shule ya Msingi ya Sinza Maalum jijini Dar es Salaam.

 
Wananchi wanaoishi Mtaa wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wameliomba Shirika la Umeme Wilaya ya Kinondoni (Tanesco) Kufika haraka  kwa ajili ya kuiondoa nguzo ya umeme iliyoanguka tokea jana jioni.

Tatizo la kuanguka kwa Nguzo hiyo limetokea katika barabara ya Kijitonyama kupitia katika shule ya Msingi ya Sinza Maalum ama mtaa uliopo nyuma ya kituo cha Polisi cha Kijitonyama “Polisi Mabatini”.


Mmoja wa wakazi anayeishi maeneo hayo akizungumza na mtandao huu amesema kuwa kwa kupitia namba zao za huduma kwa mteja wamejaribu kuwapigia lakini simu zao zinaita bila kupokelewa.


“Tunaomba jamani sisi wakazi wa eneo hili tokea jana jioni umeme umekatika, ukizingatia nguzo zimeanguka katikati mwa barabara na bado zinaumeme, tunaomba wahusika mje kuziondoa kabla madhara makubwa hayajatokea maana linaweza kutokea tatizo kubwa hasa kwa waendeshaji wa vyombo vya moto” alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu.


Kwa upande wa mkazi mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Pili Mtaturu amesema ” Tunawaomba Tanesco mje haraka maana leo ni siku ya sikukuu na wengine tunahitaji kupika kwa ajili ya sikukuu sasa kama umeme umekatika sijui tutatumia nini? alihoji huku akidai yeye amejaribu kuwapigia tokea jana wakadai wangelienda lakini hadi leo asubuhi Desemba 25 hawajafika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top