EMMANUEL Okwi mshambuliaji wa kikosi cha Al-Ittihad ya Misri amekutwa na Virusi vya Corona hivyo atakosa mechi kadhaa ndani ya Ligi Kuu ya Misri.
Raia huyo wa
Uganda ambaye amecheza pia Ligi Kuu Bara ambapo alicheza ndani ya Simba kwa
wakati tofauti pia alicheza kikosi cha Yanga atakosa mchezo pia dhidi ya
Pyramids FC baada ya kukutwa na Corona.
Mabosi wa
Al-Ittihad wamethibitisha kwamba Okwi ana Corona na hayupo nchini Misri kwa
sasa bado yupo Uganda.
“Safari ya
kurejea kwa mshambuliaji wetu ambaye anacheza timu ya taifa ya Uganda
imesimamishwa baadaye kukutwa na Corona.
“Matokeo hayo
ameyapata akiwa nchini Uganda kwani bado hajarejea nchini Msiri nasi
tunamuombea apone haraka,” ilieleza taarifa ya klabu.
Okwi alikuwa
na kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kilichokuwa zikisaka tiketi ya kufuzu
Afcon ambapo timu yao ipo kundi B.
Post a Comment