} });
 

 

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao ya biashara ili kuweza kuziuzia nchi zinazokabiliwa na janga la Corona, huku akimtaka mkandarasi wa daraja la Kigongo Busisi kuimaliza kazi hiyo ndani ya miaka mitatu na sio miaka minne.

 

Rais Magufuli amesema hayo leo (jana) Jumatatu, Desemba 28, 2020 wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika daraja hilo linalotarajia kukamilika kwa gharama ya bilioni 700.

 

“Watanzania tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona na tulime kwa nguvu zote ili kukuza uchumi wa nchi na watu kwa ujumla,mazao mtakayolima tutaziuzia nchi zinazokabiliwa na Corona maana watu wao hawafanyi kazi wapo kwenye karantini,” amesema Magufuli.

 

Amesema wananchi walime sana maana mwakani nchi inaweza kukabiliwa na janga la njaa,kutokana na nchi nyingi zitahitaji chakula kutoka Tanzania.

 

Aidha, Magufuli amemtaka mkandarasi wanayejenga daraja la Kigogo Busisi wa Kampuni ya China Civil Engineering Group Limited kwa gharama ya Tsh. bilioni 700, kujenga miradi huo usiku na mchana ili kukamilisha ndani ya miaka mitatu, maana ilitakiwa iishie.kwa muda wa miaka minne.

 

Daraja hilo la Magufuli lenye urefu wa kilo mita 3.2 na barabara unganishi 1.66 kilo mita, ambalo ni la kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi wao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top