} });
 


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli, ameahirisha sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambayo huadhimishwa Desemba 9 kila mwaka, na kuagiza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo zitumike kununulia vifaa mbalimbali vya Hospitali ya Uhuru iliyopo Dodoma.

 

Taarifa hiyo imetolewa Desemba 3, 2020, na Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa, na kusema kuwa Rais Dkt. Magufuli, ameagiza kiasi cha shilingi milioni 835,498,700, zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe za maadhimisho ya 59 ya Uhuru wa Tanzania Bara, zitumike kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya hospitali hiyo.Novemba 20, 2018, Rais Dkt. Magufuli, aliagiza kiasi cha shilingi milioni 995,182,000.00, zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho ya 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, tarehe 9 Desemba, zitumike kujenga Hospitali ya Uhuru, ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.

 

Kauli mbiu ya maadhimisho ya 59 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka huu inasema, “Miaka 59 ya Uhuru na Miaka 58 ya Jamhuri: Tanzania yenye Uchumi Imara Itajengwa na Watanzania Wenyewe, Tufanye Kazi kwa Bidii, Uwajibikaji na Uadilifu."

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top