} });
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa familia za Watu 14 waliofariki kwenye ajali ya barabarani jana Dec. 13 Kijiji cha Mkiwa Ikungi Singida baada ya Basi dogo toka Mwanza – Itigi kugongana na lori la mizigo likitokea Dar kwenda Kahama Shinyanga.

 

“Nawapa pole wafiwa wote mwenyezi mungu awatie nguvu, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wenu nawaombea marehemu wote wapumnzishwe mahala pema peponi” amesema Mhe Rais Magufuli.

 

Rais Magufuli amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuongeza jitihada za kuthibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha kufunga mwaka ambapo kumekuwa kunatokea ajali nyingi za barabarani na pia amewataka watumiaji wote  wa barabara  kuwa makini na kujiepusha na kuvunja sheria


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top